Kesi inayomkabili Mbunge wa Singida
Mashariki (Chadema), Tundu Lissu na wahariri wa Gazeti la Mawio katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeahirishwa hadi Februari 26.
Wakili wa Serikali, Elia Athanas jana
alimueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kuwa kesi imepangwa kwa ajili
ya kutajwa na kwamba hadi sasa hawajajua hali ya mshtakiwa wa nne,
Lissu.
Kesi hiyo ambayo ipo katika hatua ya
usikilizwaji wa ushahidi wa upande wa mashtaka, inamkabili Lissu na
wenzake Simon Mkina, Jabir Idrisa na Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana,
Ismail Mehbooh.
