Serikali imesitisha utoaji wa pasi za
kusafiria ‘passport’ za jumla za makundi mpaka pale utakapopatikana
utaratibu rasmi na mzuri kati ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na serikali ya nchi husika.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Dkt Mwigulu Lameck Nchemba kufuatia kuwepo kwa mikasa ya
kunyanyaswa, kutumikishwa na kuteswa kikatili kwa baadhi ya watanzania
wanaokwenda nje ya nchi kwa jili ya kufanya kazi mbalimbali ikiwemo kazi
za ndani.


